BIASHARA YA USAMBAZAJI VYAKULA MAJUMBANI INAYOFANYWA NA MWANADADA PETRONILLAH JOHN WA PETIT FOOD SU

Muda Ilipowekwa : 2018-02-13 04:12:02


Bi Petronillah John ni mwanadada aliyeamua kujiajiri kwa kubuni biashara ya usambazaji vyakula majumbani ili kumpunguzia mteja usumbufu wa kuzunguka sokoni kutafuta mahitaji. Anaamini kuwa kupitia ujasiriamali amepata fursa kubwa ya kutengeneza kipato zaidi akilinganisha na alipokua mwajiriwa kabla ya biashara hii.